Monday, 27 April 2015
Ommy Dimpoz Aikana 'KICK' ya Wema Sepetu ,Adai Hawezi kuwa Mapenzini na Wema Kwasababu Anaweza Kuharibu Mambo yake ya Maana
Msanii mkubwa Bongo Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amesema kuwa hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wema Sepetu kwa sababu anaweza kuharibu mambo yote ya maana ambayo anapanga kuyafanya.
Dimpoz aliweka wazi hayo kwa Dia wa ala za Roho na kusema kuwa Wema ni staa na ni mzuri hana tatizo lakini mazingira yanachangia awe mbali nae kwani akiweka mapenzi kutakuwa hakuna kazi.
"Unajua ukiwa na rafiki alafu mkaweka mapenzi basi patakuwa hakuna kazi zaidi ya kuharibu kazi , hata kama palikuwa na project basi mwishowe inaharibika, Nasisitiza sina uhusiano wa kimapenzi na Wema Sepetu" Alisema Dimpoz
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment