Mwanamuziki wa band ya Fm Academia Patcho Mwamba ambae pia ni muigizaji wa filamu, amejibu swali aliloulizwa kwenye mahojiano maalumu na Bestizzo "Je unahisi Wema halitendei haki jina lake au kuna sehemu anakosea?"
''Kwanza tuseme ukweli wa Mungu hamna star wa kike ana nyota kama ya Wema Sepetu, ni star ni star ni star ni star sana upande wa wanawake wote ndani ya bongo ila dhambi yake moja ni kuanika sana maisha yake... akiwa na mpenzi jamani mpenzi wangu ndio huyu hapa akiachana nae ni rahisi watu kujua...''